Umuhimu wa afya ya akili kwa watoto na vijana
2021-10-29 09:12:04| CRI

Kupunguza hatari ya watoto kuwa na matatizo ya kisaikolojia_fororder_VCG111326784697

Kutokana na mabadiliko ya kasi ya mazingira ya kijamii na kiuchumi, shinikizo kwa watoto na vijana limeongezeka, na suala la saikolojia kwa vijana limekuwa changamoto kubwa isiyopuuzwa. Vijana karibu elfu 46 duniani wanajiua kila mwaka, na kujiua ni moja kati ya sababu tano kuu za vifo vya vijana kati ya umri wa miaka 10 hadi 19. Inakadiria kuwa, zaidi ya 13% ya vijana wenye umri kati ya miaka 10-19 wana matatizo ya afya ya akili kama ilivyothibitishwa na WHO. Vilevile katika nchi zenye kipato cha juu na ya kati, karibu asilimia 20 ya vijana wenye umri kati ya miaka 15-24 haana furaha na hawana hamu ya kufanya kazi. Katika kipindi cha leo tunafuatilia matatizo ya saikolojia ya watoto.