Marekani yaipinga vikali Israel kwa kupanua ujenzi wa makazi kwenye Kando ya Magharibi ya Mto Jordan
2021-10-27 09:18:06| cri

Marekani imeeleza kupinga vikali mpango wa Israel wa kupanua ujenzi wa makazi ya walowezi wa kiyahudi katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani Ned Price amesema, mpango huo unakwenda kinyume na juhudi za kupunguza mvutano na kuhakikisha utulivu, na pia unakwamisha mafanikio ya kupata suluhu ya kuwepo kwa mataifa mawili. Ameongeza kuwa Marekani itaendelea kufuatilia suala hili moja kwa moja na maofisa wa ngazi ya juu wa Israel kwenye majadiliano ya ndani.

Israel Jumapili ilitoa zabuni kwa ajili ya ujenzi wa nyumba mpya 1,355 katika makazi yaliyopo Ukingo wa Magharibi, sambamba na ujenzi wa makazi zaidi ya 3,000 utaendelezwa wiki hii katika maeneo ya Wapalestina yanayokaliwa kwa nguvu.