Mkurugenzi mkuu wa kulinda amani wa UM asifu hatua ya kuwapunguza askari wa tume ya Abyei
2021-10-28 09:22:40| cri

Mwakilishi wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia operesheni za amani Bw. Jean-Pierre Lacroix ameendelea kuwa na mtazamo chanya juu ya uwezekano wa kupunguza askari wa kikosi cha kulinda amani huko Abyei, eneo lenye mgogoro lililoko kati ya mpaka  wa Sudan na Sudan Kusini.

Amesema ingawa Sudan na Sudan Kusini bado zinakabiliwa na changamoto za ndani, lakini bado kuna makubaliano kati ya pande mbili juu ya ushirikiano wa masuala makuu. Hali ya kisiasa ya Abyei inaonekana kuwa na matumaini. Sudan na Sudan Kusini zimeunda kamati za taifa juu ya suala la Abyei, na uhusiano wa nchi hizo mbili juu ya eneo hilo unatarajiwa kuwa mzuri. Ameongeza kuwa sasa ni mapema kujua athari ya mapinduzi ya kijeshi yaliyotokea wiki hii nchini Sudan yanamaanisha nini kwa kikosi cha muda cha usalama cha Umoja wa Mataifa huko Abyei (UNISFA).