Rais Xi Jinping wa China asema China inaikaribisha Guinea ya Ikweta kujiunga na Mpango wa Maendeleo Duniani
2021-10-28 09:41:20| cri

Rais Xi Jinping wa China amesema kwamba China inaikaribisha Guinea ya Ikweta kujiunga na Mpango wa Maendeleo Duniani.

Katika mazungumzo yake kwa njia ya simu na mwenzake wa Guinea ya Ikweta Teodoro Obiang Nguema Mbasogo, rais Xi amesema kuwa nchi yake iko tayari kushirikiana na Guinea ya Ikweta na nchi nyingine za Afrika ili kukuza maendeleo endelevu na ya pamoja ya nchi zinazoendelea.

Rais Xi ameongeza kuwa katika miaka ya hivi karibuni, uhusiano kati ya China na Guinea ya Ikweta umedumisha maendeleo ya kiwango cha juu, huku uaminifu wa kisiasa ukiwa imara na ushirikiano wao ukizaa matunda.

China inasifu sana uungaji mkono mkubwa wa Guinea ya Ikweta katika masuala yanayohusiana na Taiwan, Hong Kong, Xinjiang na haki za binadamu.