Kipindi cha Daraja kinachokujia kutoka Idhaa ya Kiswahili ya Shirika Kuu la Utangazaji la China (CMG) kinakufahamisha mambo mbalimbali kuhusu uhusiano, ushirikiano na mawasiliano kati ya China na Afrika. Katika kipindi cha leo, licha ya habari za wiki hii zilizohusisha China pamoja na nchi za Afrika, tutakuwa na ripoti kuhusu ushirikiano kati ya China na Afrika katika masuala ya kisayansi ya kukabiliana na changamoto za kimazingira. Pia tutakuwa na mahojiano kutoka CMG Idhaa ya Kiswahili Nairobi na Daktari Sabella Kiprono aliyesoma nchini China.