China yataka US isitoe ishara mbaya kwa wanaotafuta "uhuru wa Taiwan"
2021-10-28 13:00:49| cri

China yataka US isitoe ishara mbaya kwa wanaotafuta "uhuru wa Taiwan"_fororder_台湾

China imeitaka Marekani isitoe ishara mbaya kwa watu wanaotafuta “uhuru wa Taiwan” na kuchukua hatua halisi za kudumisha msingi wa kisiasa wa uhusiano kati ya China na Marekani.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Zhao Lijian amesema hayo alipozungumzia taarifa iliyotolewa na waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken kuhusu “kuunga mkono Taiwan kujiunga kwa maana kwenye mfumo wa Umoja wa Mataifa”.

Zhao amesema taarifa hiyo ya Marekani imeingilia vikali kanuni ya kuwepo kwa China moja na taarifa tatu za pamoja za China na Marekani. Kwenda kinyume na ahadi ilizotoa Marekani na taratibu za kimsingi za mahusiano ya kimataifa, ni ishara zenye makosa kwa watu wanaotafuta “uhuru wa Taiwan”. Amesema nchi 180 duniani ikiwemo Marekani zimeanzisha uhusiano wa kibalozi na China katika msingi wa kukubali kanuni ya kuwepo kwa China moja ambayo hairuhusiwi kutatizwa au kupinduliwa na Marekani.

Amesisitiza kuwa ushiriki wa Kisiwa cha Taiwan katika shughuli za mashirika ya kimataifa unatakiwa kujadiliwa kuendana na kanuni ya kuwepo kwa China moja.