Taasisi ya Confucius katika Chuo Kikuu cha Zambia yafanya maonesho ya ajira ili kuyasaidia makampuni ya China kutafuta wafanyakazi
2021-10-28 09:41:51| cri

Taasisi ya Confucius katika Chuo Kikuu cha Zambia UNZA kimeandaa maonesho ya nne ya ajira, ambapo makampuni ya China yenye makao yao nchini humo yalishiriki na kujaribu kuwavutia wafanyakazi wa huko, haswa wanafunzi watakaohitimu.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Confucius Sande Ngalande amesema taasisi hiyo ina nia ya kuhakikisha ushirikiano na viwanda unaendelea kuwepo bila ya kuathiriwa na janga la COVID-19.

Amesema maonesho hayo ni jukwaa ambalo taasisi za elimu ya juu zikishirikiana na viwanda zinatoa  watu wenye ujuzi mkubwa ambao unahitajika katika makampuni ili kuongeza ufanisi na ukuaji wa uchumi.

Grace Tembo ambaye ni kaimu mkuu wa kitivo katika UNZA, amesema maonesho hayo yametoa fursa kwa watafutaji wa ajira kupata ajira wanaozipenda na kuanza safari mpya ya kazi.