Mjumbe maalumu wa UM atoa wito wa kuondoa vikwazo vilivyowekwa na nchi za magharibi dhidi ya Zimbabwe
2021-10-28 09:21:54| cri

Katibu maalumu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia hatua za kulazimisha za upande mmoja Bibi Alena Douhan ametoa wito wa kuondoa vikwazo vilivyowekwa na nchi za magharibi dhidi ya Zimbabwe, na kutaka pande husika zifanye mazungumzo.

Douhan alisema hayo kwenye taarifa yake aliyoitoa jana baada ya kumaliza ziara ya siku kumi nchini Zimbabwe ili kutathmini athari ya vikwazo. Anapanga kutoa hotuba kwenye mkutano na wanahabari utakaofanyika leo mjini Harare, na baadaye kuwasilisha ripoti kwenye Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa mwezi Septemba mwaka 2022.

Amesema vikwazo vya upande mmoja na kuwekewa vikwazo kwa muda mrefu vimeiletea Zimbabwe changamoto nyingi zaidi kwenye sekta za kijamii na kiuchumi, na kuwaletea wananchi wa Zimbabwe hasara kubwa. Marekani na nchi nyingine husika zinapaswa kuondoa vikwazo hivyo dhidi ya watu binafsi na mashirika.