Msimu ujao wa mvua chache unatishia usalama wa chakula nchini Tanzania
2021-10-28 09:39:07| cri

TMA yasema msimu ujao wa mvua chache unatishia usalama wa chakula nchini Tanzania_fororder_坦桑

Mamlaka ya Hali ya Hewa ya Tanzania (TMA) imesema msimu ujao wa mvua chache unaweza kusababisha mavuno machache ya mazao, na kutishia usalama wa chakula nchini humo.

TMA imesema kwenye utabiri wake wa hali ya hewa, msimu wa mvua chache unatarajiwa kuanza katika wiki ya tatu ya mwezi Novemba 2021 ambao utaendelea hadi wiki ya tatu ya Aprili 2022. Kutokana na mvua za chini ya kiwango na za kiwango cha kawaida zinazotarajiwa kunyesha katika maeneo mengi ya nchi yanayoingia kwenye msimu, utashuhudiwa upunguaji mkubwa wa unyevu kwenye udongo na kuathiri ukuaji wa mazao.

Mbali na hayo msimu huo pia utakabiliwa na ongezeko la wadudu wa mazao kama vile mchwa, vimelea, panya na magonjwa, na kuathiri mazao na uzalishaji kwa ujumla. Hivyo TMA imewashauri wakulima kutumia njia endelevu za kilimo pamoja na teknolojia kwa ajili ya kulinda maji na unyevu wa udongo.