Jeshi la China latuma askari elfu 50 wa kulinda amani
2021-10-29 09:42:01| cri

Jeshi la China latuma askari elfu 50 wa kulinda amani_fororder_维和

Msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya China Tan Kefei amesema katika miaka 30 iliyopita, jeshi la China limeshiriki katika operesheni 25 za kulinda amani za Umoja wa Mataifa, na kutuma askari karibu elfu 50.

Tan amesema hayo katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika tarehe 28.

Amesema askari wa kulinda amani wa China wamesifiwa sana na pande mbalimbali kwa kutojali hatari na matatizo, kutekeleza majukumu kwa makini, kusimamia usimamishaji vita, kulinda usalama wa raia, kutuliza hali ya nchi, kusambaza mbegu za matumaini, na kutoa mchango kwa ajili ya kuhimiza amani na kuhakikisha maendeleo ya uchumi na jamii za nchi husika.

Pia amesema baada ya kuingia katika zama mpya, jeshi la China litaunda kikosi chenye askari elfu nane wanaojiandaa kutumwa, ili kuongeza nguvu katika kuunga mkono na kushiriki katika operesheni za kulinda amani za Umoja wa Mataifa.