China yapinga nchi yoyote yenye uhusiano wa kibalozi kuwa na mawasiliano ya kiserikali na Taiwan
2021-10-30 16:24:24| Cri

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Wang Wenbin amesema China inaitaka serikali ya Lithuania kufuata kwa makini ahadi ya kisiasi iliyoa ilipojenga uhusiano wa kibalozi na China na kutofanya makosa yanaweza kuleta matokeo mabaya.

Bw. Wang amesema hayo baada ya Umoja wa Ulaya kusema uamuzi wa Lithuania wa kuwekeana ofisi na Taiwan hauendi kinyume na sera ya kuwepo kwa China moja, na Umoja huo haukubali shinikizo kutoka kwa serikali ya China. Bw. Wang amesisitiza kuwa sera ya kuwepo kwa China moja ni msingi wa kisiasa wa China kuanzisha uhusiano wa kibalozi na nchi nyingine, na inapinga nchi yoyote yenye uhusiano wa kibalozi na China kuwa na mawasiliano ya kiserikali na Taiwan.