Rais wa China atoa hotuba kwenye mkutano wa G20
2021-10-30 20:56:49| Cri

Rais Xi Jinping wa China kwa njia ya video amehudhuria na kutoa hotuba kwenye kikao cha kipindi cha kwanza cha mkutano wa wakuu wa nchi za kundi la G20.

Rais Xi amesema wakati dunia inakabiliwa na mabadiliko makubwa na janga la COVID-19, kundi hilo likiwa ni baraza kubwa la uchumi la kimataifa linapaswa kubeba wajibu, kushikilia uwazi na ujumuishi, kushirikiana na kutafuta mafanikio kwa pamoja, kutekeleza utaratibu wa pande nyingi na kuhimiza ujenzi wa jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja.
Rais Xi ameongeza kuwa China itatoa fursa mpya kwa nchi mbalimbali na kuchangia nguvu zaidi kwa uchumi wa dunia.