Rais Xi aweka lengo la kuongeza usawa, ufanisi na ushirikishi wa maendeleo ya dunia katika Mkutano wa G20
2021-10-31 13:19:51| Cri

Rais Xi Jinping wa China ameweka lengo la kushikilia kutoa kipaumbele cha wananchi, kuongeza usawa, ufanisi na ushirikishi wa maendeleo ya dunia, na kutoacha nchi yoyote katika mchakato wa maendeleo katika Mkutano wa kilele wa G20 uliofunguliwa tarehe 30 mjini Rome, Italia.  

Akihutubia mkutano huo, rais Xi alitoa mapendekezo matano: kufanya mshikamano na ushirikiano, na kupambana kwa pamoja na janga la Corona; kuimarisha uratibu na kuhimiza ufufukaji wa uchumi; kunufaisha na kushirikisha pande zote, na kupata maendeleo kwa pamoja; kufanya uvumbuzi na kutafuta msukumo mpya; kuishi kwa masikilizano, na kupata maendeleo endelevu ya kijani.