Wizara ya Mambo ya Nje ya China yapinga ripoti ya Marekani kuhusu chanzo cha virusi vya Corona
2021-10-31 14:45:15| Cri

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Wang Wenbin amepinga ripoti kuhusu chanzo cha virusi vya Corona iliyotolewa na shirika la ujasusi la Marekani, akisema kuwa uwongo unaorudiwa mara elfu kadhaa bado ni uwongo, na kwamba haiwezi kubadilisha ukweli kwamba ripoti hii ni ya kisiasa na yenye uwongo, na haina msingi wa kisayansi tena haiaminiki.

Wang amesema ufuatiliaji wa chanzo cha virusi vya Corona ni suala muhimu la kisayansi, na linapaswa tena linaweza tu kuchunguzwa kwa ushirikiano na wanasayansi kote duniani. Kuyafanya mashirika ya ujasusi kutafuta chanzo cha virusi vya Corona ni shahidi la kulifanya suala hilo kuwa la kisiasa.

Amesisitiza kuwa kile Marekani kinachopaswa kufanya kwa sasa ni kuacha kukwepa lawama na kuzingatia mapambano dhidi ya janga la virusi nchini na kufanya ushirikiano wa kimataifa.