Zaidi ya wanariadha 1,000 wa ridhaa wafuzu kushiriki mbio za Marathon za Paris 2024 kwa “kumshinda” Kipchoge
2021-11-01 09:16:02| CRI

Zaidi ya wanariadha 1000 wa ridhaa wamejipatia nafasi ya kushiriki kwenye mbio za marathon zinazohusiana na michezo ya Olimpiki ya mwaka 2024, baada ya kumaliza changamoto ya “kumshinda” bingwa wa Olimpiki mara mbili Eliud Kipchoge kwenye mbio maalum zilizofanyika mjini Paris.

Mbio hizo za kilometa 15 zilifanyika kwenye eneo la ikulu ya Ufaransa kusherehekea siku 1,000 kabla ya kuanza kwa michezo ya Olimpiki ya Ufaransa.

Kwenye mbio hizo zaidi ya wanariadha 3,600 walijitokeza, na kutangulia kukimbia huku Eliud Kipchoge akianza akiwa wa mwisho, na wote alioshindwa kuwapita katika mbio hizo wametajwa kuwa ni washindi, na wamefuzu kushiriki kwenye mbio za marathon kwenye michezo ya Olimpiki ya Paris.