Rais Xi Jinping aendelea kushiriki kwenye Mkutano wa 16 wa Kilele wa Kundi la Nchi 20
2021-11-01 09:08:09| CRI

Rais Xi Jinping aendelea kushiriki kwenye Mkutano wa 16 wa Kilele wa Kundi la Nchi 20_fororder_2021110100171394362

Rais Xi Jinping wa China ameendelea kushiriki kwenye Mkutano wa 16 wa Kilele wa Kundi la Nchi 20 (G20) kwa njia ya video, ambapo amefafanua maoni yake juu ya masuala ya mabadiliko ya tabianchi, nishati na maendeleo endelevu.

Rais Xi Jinping amesema, mabadiliko ya tabianchi na suala la nishati ni changamoto kubwa zinazoikabili dunia nzima, na kuitaka jumuiya ya kimataifa ichukue hatua za kisera zilizo kamili na zenye uwiano, kutekeleza kwa ufanisi Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Tabianchi na Makubaliano ya Paris, na kuongeza uungaji mkono kwa nchi zinazoendelea, ili kukabiliana kwa pamoja na changamoto hizo.

Rais Xi amesisitiza kuwa hivi karibuni China imetoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuharakisha utekelezaji wa Ajenda ya Umoja wa Mataifa ya Maendeleo Endelevu ya mwaka 2030, na kusukuma mbele maendeleo ya kijani duniani. Rais Xi amelitaka kundi la G20 litoe kipaumbele kwa maendeleo na kutanguliza maslahi ya umma, na kuhimiza ushirikiano halisi na wa kunufaishana, ili kujenga jumuiya ya binadamu yenye mustakbali wa pamoja wa maendeleo.