Serikali ya Ethiopia yasema kundi la TPLF limewaua raia zaidi ya 100 wa kawaida katika jimbo la kaskazini
2021-11-02 09:58:30| CRI

Serikali ya Ethiopia imeeleza kuwa raia zaidi ya 100 wameuawa na kundi la waasi katika wilaya muhimu ya jimbo la Amhara la nchi hiyo.

Huduma ya mawasiliano ya serikali ya nchi hiyo imesema, kundi la kigaidi la TPLF limewaangamiza vijana zaidi ya 100 ambao ni wakazi wa Kombolcha katika maeneo waliyojipenyeza, huku ikitoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kutopuuza ukatili huo.

Msemaji wa serikali ya Ethiopia Legesse Tulu amesema, kikosi kinachoitii TPLF kiliwalenga vijana wa Kombolcha. Kombolcha ni mji muhimu wa viwanda wa mkoa wa Amhara unaopakana na mko wa Tigray ulioathiriwa vibaya na mapigano.

Kabla ya hapo, baraza la chini la bunge la Ethiopia lililiweka kundi la TPLF katika orodha ya makundi ya kigaidi.