Kenya kupeleka ujumbe wa wafanyabiashara nchini DRC kuhimiza biashara za pande mbili
2021-11-02 09:57:52| CRI

Kenya imetangaza kuwa itaunda ujumbe wa wafanyabiashara kwa ajili ya jamii yake ya wafanyabiashara kwenda nchini DRC, ili kuhimiza biashara ya pande mbili.

Waziri wa Biashara, Viwanda na Maendeleo ya Kampuni wa nchi hiyo Bi. Betty Maina amewaambia wanahabari huko Nairobi kuwa, ujumbe huo utafanya ziara ya siku 15 nchini DRC kuanzia Novemba 29 hadi Desemba 13 katika miji ya Kinshasa, Lubumbashi, Goma na Mbuji Mayi.

Maina amesema, DRC ni nchi ya sita duniani inayoongoza katika kuuza bidhaa za Kenya, ambapo bidhaa za kilimo na utengenezaji zikiwa juu kwenye orodha. Ujumbe huo wa wafanyabiashara utaimarisha huduma na uwekezaji wa bidhaa kati ya nchi hizo mbili, na kutarajiwa kutafuta fursa nyingi zaidi katika sekta mbalimbali za uchumi.