Lugha kama chombo cha mawasiliano hutumika kama daraja baina ya jamii na jamii nchi na nchi au hata bara na bara. Lugha za Kiswahili na Kichina kwa sasa zimeleta manufaa kwa wazungumzaji wa pande zote mbili, na wengi wao sasa wamekuwa na ari na hamu ya kutaka kujifunza lugha hizi kwani zinawasaidia katika biashara zao, shughuli za utamaduni au hata mawasiliano wakati wanapotembeleana.