Gavana wa jimbo la Nigeria aahidi uchunguzi kamili kufuatia jengo kuporomoka
2021-11-03 09:29:49| CRI

Gavana wa jimbo la Lagos ameahidi uchunguzi kamili kufanyika kuhusu ajali ya jengo lililoporomoka ambayo ilitokea Jumatatu alasiri mjini Lagos.

Babajide Sanwo-Olu, gavana wa jimbo la Lagos, alisema kupitia taarifa Jumanne kuwa serikali ya jimbo hilo inaunda jopo huru ili kuchunguza ajali ya kuanguka kwa jengo lenye ghorofa 21 kwenye eneo la Ikoyi mjini Lagos Jumatatu, ambayo mpaka sasa imesababisha vifo vya watu 15.

Gavana huyo amesema wajumbe wa jopo hilo watatoka kwenye taasisi za kitaalumu katika nyanja ya ujenzi, kama vile Taasisi ya Nigeria ya Wasanifu Majengo, Tassisi ya Nigeria ya Mipango Miji, na Jumuiya ya Wahandisi ya Nigeria.

Gavana huyo amesema serikali itachunguza chanzo cha tukio hilo na kuwafikisha wahusika mbele ya sheria, na katika hatua ya kwanza, ameagiza meneja mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Majengo Jimbo la Lagos asimamishwe kazi mara moja.