Naibu spika wa bunge la Afrika Kusini atarajia Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Bairidi ya Beijing itaionyesha dunia sura bora ya China
2021-11-03 11:10:12| CRI

Naibu spika wa bunge la Afrika Kusini atarajia Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Bairidi ya Beijing itaionyesha dunia sura bora ya China_fororder_Tsenoli

Naibu spika wa Bunge la Afrika Kusini Bw. Solomon Lechesa Tsenoli hivi karibuni alipohojiwa na Shirika Kuu la Utangazaji la China CMG amesema ana matarajio makubwa na Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing. Anaona michezo inaweza kuvuka tofauti na kuwaleta watu pamoja, na michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi ya Beijing si kama tu itakuwa na umuhimu maalumu katika kuondoa maumivu ya janga la virusi vya Corona na kukusanya nguvu za dunia, na bali pia itafungua dirisha kwa dunia kuikaribia na kuielewa vizuri zaidi China na utamaduni wake. Bw. Tsenoli anatarajia kuwa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing itaionyesha dunia sura bora ya China.

Akiwa mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha Afrika Kusini, Bw. Tsenoli ana uelewa wa kina kuhusu Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na maendeleo ya China. Amesema, sio jimbo la kawaida katika dunia nzima kwa chama kimoja cha siasa kudumu kwa miaka zaidi ya mia moja na kuendelea kustawi. Sabubu moja muhimu iliyoifanya CPC kustawi baada ya kuwepo kwa miaka mingi ni kuwa kimedumisha uhusiano wa karibu na umma, kutegemea busara za umma, kuhamasisha nguvu na ari ya umma, na kuboresha maisha ya watu. Amesema, ni kutokana na uongozi wa CPC, China imeweza kutimiza maendeleo ya kasi ya uchumi na utulivu wa kudumu katika jamii. Bw. Tsenoli amepongeza mafanikio makubwa ya CPC ya kuwaongoza mamilioni ya watu kuondokana na umaskini, kutokana na msimamo wake thabiti wa kisiasa na mbinu sahihi za kisayansi.

Kwa mtizamo wa Bw. Tsenoli, China si kama tu imetimiza maendeleo yake yenyewe, na bali pia inatoa fursa nyingi kwa nchi nyingine duniani. Bw. Tsenoli amepongeza nafasi muhimu ya China katika jukwaa la kimataifa. Amesema huu ni mwaka wa 50 tangu China irejeshewe kiti chake halali katika Umoja wa Mataifa, katika miaka hiyo 50 iliyopita, China imekuwa ikijiendeleza kwa amani na kujitahidi kunufaisha binadamu wote. Bw. Tsenoli amesema, baadhi ya nchi siku zote zimekuwa zikijaribu kuzuia mchakato wa kuyafanya mahusiano ya kimataifa yawe ya kidemokrasia, lakini China siku zote imekuwa ikisimama bega kwa bega na nchi za Afrika, kutetea hadhi na mamlaka ya Umoja wa Mataifa na kulinda kwa pamoja mifumo ya pande nyingi.

Bw. Tsenoli pia amesifu dhana ya Jumuiya ya Binadamu yenye Hatma ya Pamoja iliyotolewa na China, na kuona dhana hii inalingana na falsafa ya Afrika inayotaka mahusiano ya kuheshimiana, na kuonyesha mtizamo wa China ulio wazi na shirikishi wa kukumbatia staarabu anuwai za dunia. Amesema uhuru na demokrasia ni malengo ya pamoja ya binadamu wote, ambayo hayatakiwi kuamuliwa na kupewa maudhui na nchi chache. Baadhi ya nchi zinajaribu kulinda hadhi yao ya umwamba duniani kwa kisingizio cha “demokrasia”, na hii sio demokrasia ya kweli. Bw. Tsenoli amesema, anatarajia kuwa Afrika Kusini itaimarisha ushirikiano na China kwenye mifumo ya pande nyingi ya kimataifa, ili kuuwezesha Umoja wa Mataifa kupaza zaidi sauti za nchi zinazoendelea.

Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) lililoanzishwa zaidi ya miaka 20 iliyopita, limeonyesha kikamilifu uungaji mkono thabiti wa China kwa maendeleo na ustawi wa Afrika. Bw. Tsenoli amesema, Afrika Kusini, sawa na nchi nyingi za Afrika, imenufaika pakubwa kutokana na mawasiliano na ushirikiano kati yake na China, haswa katika nyanja ya ujenzi wa uwezo na uendelezaji wa viwanda. Ameeleza matarajio yake makubwa kwa mkutano ujao wa kilele wa FOCAC utakaofanyika mwaka huu nchini Senegal. Amesema, ujenzi wa Eneo la Biashara Huria la Afrika AfCFTA ulizinduliwa rasmi mwaka huu, na kuimarisha ushirikiano kati ya Afrika na China na kati ya Afrika Kusini na China katika hali hii kuna umuhimu mkubwa. Bw. Tsenoli amesema anatumia kuwa chini ya msaada wa China, Afrika itaweza kuongeza zaidi uwezo wa uzalishaji na kuharakisha maendeleo ya viwanda, na pia anatarajia ushirikiano kati ya Afrika na China uendelee kuwanufaisha watu wa pande hizo mbili.