Taasisi ya Confucius nchini Uganda yafunguliwa tena baada ya kufungwa kwa miezi kutokana na COVID-19
2021-11-03 09:37:30| CRI

Taasisi ya Confucius katika chuo kikuu cha Makerere nchini Uganda imefunguliwa tena baada ya kufungwa mwezi Juni kutokana na wimbi la pili la maambukizi ya COVID-19 nchini humo.

Mkurugenzi wa taasisi hiyo Bw. Gilbert Gumoshabe amesema, masomo yameanza tena Jumatatu baada ya maelekezo ya serikali kwamba vyuo vyote vifunguliwe Novemba 1.

Amesema, kufuatia ongezeko la wagonjwa wa COVID-19 wamelazimika kusitisha mafunzo ya darasani kuanzia mwezi Juni na badala yake kutoa mafunzo kupitia mtandao wa Internet. Lakini sasa wamefungua tena ili wanafunzi waweze kushiriki masomo ya ana kwa ana darasani.

Taasisi hiyo pia imesema, kufuatia kurejea kwa masomo yote, nayo itafuata kwa makini hatua za kinga dhidi ya COVID-19.