Mshauri mwandamizi wa kisiasa wa China akutana na mwenyekiti wa seneti ya Jamhuri ya Kongo
2021-11-04 09:42:00| CRI

Mshauri mwanadamizi wa kisiasa wa China Bw. Wang Yang jana Jumatano alikutana na mwenyekiti wa seneti ya Jamhuri ya Kongo Bw. Pierre Ngolo kwa njia ya video.

Bw. Wang Yang, ambaye ni mwenyekiti wa Kamati ya kitaifa ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China (CPPCC), amesema pande hizo mbili zinapaswa kuimarisha hali ya kuaminiana kisiasa, kupanua ushirikiano halisi, kuongeza uratibu na ushirikiano kwenye masuala ya kikanda na kimataifa, na kusukuma mbele maendeleo ya kina ya uhusiano wa wenzi wa kimkakati kati ya nchi hizo mbili.Kwa upande wake Bw. Ngolo ameishukuru China kwa kuiunga mkono sana Jamhuri ya Kongo kwenye mapambano dhidi ya janga la virusi vya Corona na kusaidia maendeleo ya kiuchumi na kijamii nchini humo. Amesema Jamhuri ya Kongo itaendelea kuunga mkono zaidi masuala yanayohusu maslahi makuu ya China, na Seneti ya Kongo inapenda kuimarisha mawasiliano na ushirikiano na CPPCC ili kukuza zaidi uhusiano wa nchi hizo mbili.