Rais Xi awatunuku tuzo ya juu ya sayansi msanifu wa ndege na mtaalamu wa nyuklia
2021-11-04 09:42:34| CRI

Rais Xi Jinping wa China jana Jumatano alimtunuku tuzo ya juu ya sayansi ya China msanifu wa ndege Gu Songfen na mtaalamu wa nyuklia Wang Dazhong kutokana na michango yao mikubwa kwenye mavumbuzi ya kisayansi na kiteknolojia.

Rais Xi alitoa nishani na vyeti hivyo kwenye sherehe ya mwaka iliyofanyika Beijing ili kutoa heshima kwa wanasayansi, wahandisi na mafanikio yao kwenye utafiti.

Sherehe hiyo ya Jumatano iliyohudhuriwa na watu wapatao elfu tatu ilipongeza miradi 264 na kutoa Tuzo ya Kitaifa ya Sayansi kwa washindi 46, Tuzo ya Kitaifa ya Uvumbuzi wa Kiteknolojia kwa watu 61, na wengine 157 walitunukiwa Tuzo ya Kitaifa ya Maendeleo ya Kisayansi na Kiteknolojia.