Tanzania yapanga kujenga chuo kikuu kitakachopewa jina la baba wa taifa
2021-11-04 10:31:33| CRI

Mamlaka ya elimu Tanzania imesema, inapanga kujenga chuo kikuu kwa thamani ya dola milioni 44.5 za kimarekani kitakachopewa jina la baba wa taifa Julius Nyerere.

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Bw. Omary Kipanga amesema, chuo kikuu hicho kinachojulikana kama chuo kikuu cha kilimo na teknolojia cha Julius Nyerere kitajengwa huko Butiama.

Bw. Kipanga amesema, chuo kikuu hicho kinataka kubadilisha kilimo cha nchi hiyo kupitia matumizi ya teknolojia na watu wenye ujuzi wa hali ya juu.

Amesema, chuo kikuu hicho kitajengwa kupitia mradi wa Elimu ya Juu kwa Mabadiliko ya Kiuchumi HEET unaoungwa mkono na benki ya dunia na kulenga kusaidia kuimarisha uwezo na sifa ya vyuo vikuu vilivyochaguliwa kujenga wafanyakazi bora wenye ujuzi wa hali ya juu.