Rais Xi Jinping ahutubia ufunguzi wa Maonesho ya 4 ya CIIE
2021-11-05 09:36:04| CRI

Rais Xi Jinping wa China alihutubia kwa njia ya video ufunguzi wa Maonesho ya 4 ya Uagizaji bidhaa ya Kimataifa ya China CIIE usiku wa jana Alhamisi.

Kwenye hotuba yake, rais Xi amebainisha kuwa ufunguaji mlango ni alama wazi ya China katika zama za leo. Dhamira ya China ya kupanua ufunguaji mlango haitabadilika, dhamira ya China ya kuinufaisha dunia kwa fursa za maendeleo haitabadilika na dhamira ya China ya kusukuma mbele mafungamano ya kiuchumi ya dunia kwenye mwelekeo ulio wazi zaidi, shirikishi zaidi, wenye uwiano zaidi na wa kunufaishana, pia haitabadilika.

Rais Xi ametoa wito wa kuwepo mshikamano zaidi kati ya watu wa nchi mbalimbali duniani ili kukabiliana kwa pamoja na janga la virusi vya Corona na kuhimiza ufufuaji wa uchumi wa dunia. Amesema China inapenda kushirikiana na nchi mbalimbali katika kujenga uchumi wa dunia ulio wazi na kuinufaisha dunia nzima kwa kufuata mkondo wa ufunguaji mlango.