Mazungumzo ya kwanza ya viongozi wa baadaye kati ya China na Afrika yafanyika mtandaoni
2021-11-08 09:07:57| cri

Mazungumzo ya kwanza ya viongozi wa baadaye kati ya China na Afrika yafanyika mtandaoni_fororder_299

 Mazungumzo ya kwanza ya viongozi wa baadaye kati ya China na Afrika yanayolenga kuhimiza zaidi mawasiliano kwa kina kati ya vijana na China na Afrika yamefanyika jana kwa njia ya mtandao.

Vijana kutoka China na nchi za Afrika wamezungumzia mada kuu tatu, ambazo ni Matumaini ya Vijana: Maana ya Maendeleo ya China kwa Dunia, Nguvu za Vijana: Kuchangia Ushirikiano wa Kunufaishana na Maendeleo ya Pamoja kati ya China na Afrika, na Majukumu ya Vijana: Kujenga kwa pamoja Jumuiya yenye Hatma ya Pamoja kati ya China na Afrika.

Mkurugenzi wa Shirikisho la Urafiki la watu wa China na nchi za nje Bw. Lin Songtian amewataka vijana wa China na Afrika wawe warithi wazuri wa urafiki kati ya pande hizo mbili, na kufanya jitahidi kwa ajili ya ustawi wa nchi zao na urafiki kati ya China na Afrika.