ECOWAS yaweka vikwazo dhidi ya mamlaka ya mpito ya Mali
2021-11-08 08:57:36| cri

ECOWAS yaweka vikwazo dhidi ya mamlaka ya mpito ya Mali_fororder_webwxgetmsgimg (2)

Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Magharibi mwa Afrika (EOWAS) imetangaza vikwazo dhidi ya mamlaka ya mpito nchini Mali, kufuatia nchi hiyo kushindwa kutimiza muda wa mwisho uliowekwa wa kufanya uchaguzi ambao ni Februari mwakani.

Akisoma Taarifa ya pamoja iliyotolewa na Jumuiya hiyo baada ya Mkutano wa Tatu wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa ECOWAS kuhusu hali ya kisiasa nchini Mali na Guinea, mwenyekiti wa Kamati ya ECOWAS Jean-Claude Kassi Brou amesema, Jumuiya hiyo imeamua kuweka vikwazo dhidi ya watu na makundi yaliyotambuliwa, ikiwemo wajumbe wote wa serikali ya mpito, familia zao, na taasisi nyingine za mpito.

Jumuiya hiyo imeutaka Umoja wa Afrika, Umoja wa Ulaya, Umoja wa Mataifa na wenzi wengine wa pande mbili na pande nyingi kuridhia na kutekeleza vikwazo hivyo.