Kamati kuu ya 19 ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) yaanza kikao chake cha sita mjini Beijing
2021-11-08 14:45:43| Cri

Kamati kuu ya 19 ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) imeanza kikao chake cha sita mjini Beijing, ambapo katibu mkuu wa kamati hiyo rais Xi Jinping ametoa ripoti ya kazi kwa niaba ya ofisi ya siasa ya Kamati Kuu ya CPC na kutoa maelezo juu ya rasimu kuhusu mafanikio makubwa na uzoefu wa kihistoria wa kazi za miaka 100 za CPC.

Kikao hicho kitaendelea hadi Alhamis ambapo ofisi ya siasa pia imeamua kuwasilisha rasimu kwa ajili ya mashauriano. Wakati wa kuandika rasimu hiyo, maoni na mapendekezo kutoka ndani na nje ya chama yalikusanywa. Rais Xi pia aliongoza kongamano ili kusikiliza viongozi wa kamati kuu za vyama vingine vya kisiasa, mkuu wa Shirikisho la Wachina Wote la Viwanda na Biashara, na watu wasio na vyama vyovyote.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa baada ya mkutano wa Oktoba, CPC kimeyaongoza makabila yote nchini kufikia mafanikio katika zaidi ya miaka 100 ya historia ya maendeleo ya binadamu.