China yapinga vikali aina zote za ugaidi
2021-11-09 08:59:03| cri

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje Bw. Wang Wenbin amesema, China inalaani vikali mashambulizi ya kigaidi katika mkoa wa Tilaberg nchini Niger, na inatoa salamu za rambirambi kwa familia za wahanga wa shambulizi hilo.

Bw. Wang amesema, China inapinga kithabiti aina zote za ugaidi, na itaendelea kuunga mkono kwa dhati juhudi za serikali ya Niger za kudumisha utulivu wa kitaifa na usalama wa watu.

Habari zinasema, watu zaidi ya 80 wameuawa katika mashambulizi mawili yaliyotokea nchini Niger.