Balozi wa Tanzania ataka Wachina wajue zaidi bidhaa za Tanzania kupitia CIIE
2021-11-09 08:52:27| CRI

Balozi wa Tanzania nchini China atarajia wateja wengi zaidi wa China kufahamu bidhaa za Tanzania kupitia CIIE_fororder_QQ图片20211109085144

Maonyesho ya Nne ya Kimataifa ya Uagizaji Bidhaa ya China CIIE yanaendelea mjini Shanghai.

Balozi wa Tanzania nchini China Mbelwa Kairuki amesema hivi karibuni kuwa, anatarajia wateja wengi zaidi wa China watafahamu bidhaa za Tanzania kupitia maonesho hayo. Amesema, China imeahidi kufungua zaidi soko la bidhaa kutoka nje, hivyo Tanzania ingependa kutumia fursa hiyo kutangaza bidhaa zake kwenye soko la China. Amesema makampuni ya Tanzania yanashiriki maonesho hayo kwa njia ya mtandao, ili kutambulisha na kutangaza bidhaa mbalimbali zenye ubora wa juu nchini China, zikiwemo kahawa, korosho, mvinyo, pamoja na madini ya vito kama vile Tanzanite. 

Jumla ya nchi 58 na mashirika matatu ya kimataifa yanashiriki katika maonyesho ya kitaifa, na karibu kampuni elfu tatu kutoka nchi na sehemu 127 zimejitokeza kwenye maonyesho ya viwanda.