Waziri mkuu wa Iraq asema amewatambua washukiwa wa jaribio la kumuua
2021-11-09 08:58:14| cri

Waziri mkuu wa Iraq Mustafa al-Kadhimi jana amesema amewatambua washukiwa walioshindwa kufanya jaribio la kumuua katika makazi yake mjini Baghadad.

Amesema, washukiwa hao ni wale waliomuua ofisa wa idara ya upelelezi ya nchi hiyo Nibras Farman, na wataadhibiwa kisheria.

Jana alfajiri, al-Kadhimi alinusurika bila kujeruhiwa katika jaribio la kumuua lililofanywa na ndege isiyo na rubani katika makazi yake, ambako ziko baadhi ya ofisi za serikali na balozi za nchi za nje.

Jaribio hilo limetokea wakati kuna maandamano yanayofanywa na wafuasi wa vyama vya kisiasa kupinga matokeo ya uchaguzi.