Nchi za Afrika Mashariki zahimizwa kupitisha kiwango cha juu cha ushuru wa asilimia 35
2021-11-09 11:04:16| cri

 

 

Baraza la Biashara la Afrika Mashariki (EABC) jana limezitaka nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kupitisha pendekezo la ushuru wa asilimia 35 kuwa kiwango cha juu zaidi cha ushuru wa nje wa pamoja (CET).

Taarifa ya Baraza hilo imesema, kiwango kilichopendekezwa cha ushuru wa pamoja wa nje cha asilimia 35 ni msimamo unaoungwa na mashirikisho mengi ya wazalishaji kwenye kanda ya Afrika Mashariki

Taarifa hiyo imesema, kupitishwa kwa kiwango hicho kutahamasisha maendeleo ya viwanda, kulinda viwanda vichanga dhidi ya ushindani usio wa haki, na kulinda viwanda dhidi ya uagizaji wa bei nafuu na wa ruzuku kutoka nje, pamoja na ajira.