Habari kuhusu “mbegu za misonobari kutoka Afghanistan zauzwa haraka nchini China ” ni mwanzo tu
2021-11-09 11:20:50| Cri

Tarehe 6 usiku, katika Maonesho ya nne ya uagizaji bidhaa ya kimataifa ya China, kwenye studio maalum ya Shirika Kuu la Utangazaji la China CMG, makopo laki 1.2 ya mbegu za misonobari yaliuzwa kwa haraka. Hii ilikuwa ni moja ya habari zilizogonga vichwa vya habari kwenye mitandao ya kijamii ya China. Chini ya habari hii, wanamtandao wa China waliandika ujumbe wa kutakia kila la heri: “Ni nzuri kuweza kuwasaidia watu wanaokabiliwa na mateso ya vita”, “Nitanunua mbegu za misonobari leo usiku, maisha ya watu wa Afghanistan kweli sio rahisi”.

Sehemu ya bidhaa hizo zinatoka kwenye shehena yenye tani 45 za mbegu za misonobari iliyowasili hivi karibuni mjini Shanghai kwa ndege ya kukodi. Mwaka huu Afghanistan ilipata mavuno mazuri ya mbegu za misonobari, lakini kutokana na athari za janga la virusi vya Corona na hali ya nchini humo, ni vigumu kupata soko la uhakika nchini, hivyo China iliwafungulia wakulima wa Afghanistan “ushoroba maalumu wa angani wa kusafirisha mbegu za misonobari”, ili kusaidia kufikisha mazao yao kwenye soko kubwa la China.

Sio jambo la kushangaza kwa makopo laki 1.2 ya mbegu za misonobari kutoka Afghanistan kuuzwa kwa mkupuo kwenye maonesho ya CIIE, kwa kuwa hayo ndio matokeo ya maonesho ya CIIE kuzijengea jukwaa la mauzo nchi zinazoendelea hasa nchi zilizo nyuma zaidi kimaendeleo, na pia ni matunda ya uhakika yanayotokana na juhudi za China za kulinda mifumo halisi ya pande nyingi na kuinufaisha dunia kwa fursa za soko lake.

   Kwa mtazamo wa China, maendeleo halisi yanapatikana tu kwa pamoja, na ustawi wa pamoja ndio ustawi halisi. “Kunufaishana” iko kwenye jeni ya maonesho ya CIIE. Mwaka huu, mashirika yapatayo 90 kutoka nchi 33 zilizo nyuma zaidi kimaendeleo yameshiriki kwenye maonesho. Maonesho ya CIIE yanaweka jukwa zuri kwa nchi zilizo nyuma kimaendeleo kujiunga kwenye mfumo wa biashara ya pande nyingi. Kituo cha Biashara cha Kimataifa kilichoanzishwa kwa pamoja na Umoja wa Mataifa na Shirika la Biashara Duniani WTO chini ya usaidizi wa China, kimeweka mabanda maalumu yenye bidhaa za chakula, mazao ya kilimo na bidhaa za matumizi, kwa ajili ya kuonyesha bidhaa kutoka nchi za Afrika na Latin Amerika. Bila shaka, maonesho ya CIIE yameweka “barabara ya mwendo kasi” kwa nchi zilizo nyuma zaidi kimaendeleo kuingiza bidhaa zao kweye soko la China.

Hivi sasa, kutokana na athari za janga la Corona na mabadiliko makubwa kwenye utaratibu wa kimataifa, suala la kukosekana kwa uwiano kwenye maendeleo ya dunia limejitokeza zaidi. Katika hali hii, China kuandaa maonesho ya CIIE kama ilivyopangwa, kumezinufaisha nchi zote kwa usawa kutokana na fursa za maendeleo ya China, na kutasukuma mbele utandawazi kuelekea kwenye mwelekeo ulio wazi zaidi, shirikishi zaidi, wenye uwiano zaidi na wa kunufaishana zaidi, ambao ni muhimu sana kwa ufufuaji wa uchumi wa dunia. Katibu mkuu wa Shirika la Biashara na Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNCTAD Rebeca Grynspan ameainisha kuwa, “ China ni mshirika mkuu wa biashara kwa nchi nyingi zinazoendelea, na asilimia 20 ya uuzaji nje wa nchi zilizo nyuma zaidi kimaendeleo ulifanywa na China. Maonesho ya CIIE yamefanyika kwa mwaka wa nne sasa, na mafanikio yake makubwa ni ya kufurahisha.”

Inakadiriwa kuwa, katika China inayodhamiria kupanua ufunguaji mlango wenye kiwango cha juu, na katika uchumi wake ambao ni wa pili kwa ukubwa duniani unaoshikilia kuhimiza maendeleo ya pamoja, habari ya “mbegu za misonobari kutoka Afghanistan zauzwa haraka” ni mwanzo tu.