Iran yaapa kuongeza uwezo wa ulinzi licha ya vikwazo vya Marekani
2021-11-10 08:30:54| CRI

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Hossein Amir Aboullahian amerejea tena sera ya ulinzi ya nchi hiyo, akisema kuwa Iran itaendelea kuboresha nguvu yake ya kijeshi licha ya vikwazo vilivyowekwa na Marekani.

Akizungumza na mwenzake wa Ufaransa Jean-Yves Le Drian kwa njia ya simu hapo jana, Amir amesema, mpango wa ulinzi ni haki halali ya kila nchi, na bila ya kujali tabia isiyo ya kiujenzi ya vikwazo vya Marekani, Iran itaendelea kuongeza uwezo wa ulinzi wa jeshi la nchi hiyo.

Amesisitiza kuwa, kuna haja ya Marekani kutoa uhakikisho wa kutoweka vikwazo zaidi kwa kukiuka uwezekano wa kufikia makubaliano na udhibitisho wa uhakiki wa kuondoa vikwazo vilivyopo.

Kwa upande wake, Bw. Le Drian amesema nchi yake inaunga mkono ahadi za pande zote zinazohusika kwenye makubaliano ya nyuklia ya Iran (JCPOA), na kueleza matumaini yake kuwa, mazungumzo yajayo ya Vienna yatapata maendeleo ya kasi.