EAC yazindua jukwaa la mtandaoni ili kuunganisha vijana wenye taaluma na ajira
2021-11-10 08:25:06| cri

 

 

Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) jana imezindua jukwaa la mtandaoni linalolenga kuwaunganisha vijana wenye taaluma na ajira.

Taarifa iliyotolewa na Jumuiya hiyo imesema, jukwaa hilo la mtandaoni limezinduliwa kupitia mradi wake wa Ujuzi wa Kidijitali kwa Viwanda vya Uvumubuzi vya Afrika Mashariki.

Taarifa hiyo imesema, jukwaa hilo lilizinduliwa kwenye kilele cha viongozi wa vijana wa kikanda mwaka 2021 zilizofanyika Arusha, Tanzania.

Jukwaa hilo litaunganisha vijana wenye taaluma na biashara ili kutoa ajira, na linalenga kuziba pengo la ujuzi, hasa ujuzi wa kidijitali katika matumizi na ukuzaji wa bidhaa na huduma za kidijitali ambazo zinahitajika katika kanda hiyo.