China yanufaika na soko lake pamoja na nchi nyingine duniani
2021-11-10 08:52:04| CRI

China yanufaika na soko lake pamoja na nchi nyingine duniani_fororder_timg (50)

Mkutano wa kuadhimisha miaka 20 tangu China ijiunge na Shirika la Biashara Duniani (WTO) umefanyika mjini Shanghai.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya nje ya China Wang Wenbin amesema, China itafungua mlango zaidi, kulinda kithabiti mfumo wa biashara wa pande nyingi, na kuendelea kuimarisha ushirikiano wa biashara wa kikanda na ule ulio kati ya pande mbili.

Wang amesema, katika miaka 20 iliyopita, pato la ndani la China limeongezeka kwa mara nane, na China imekuwa nchi ya pili duniani kwa ukubwa wa uchumi, na nchi ya kwanza kwa ukubwa wa biashara, wakati huo huo China imechangia ukuaji wa uchumi wa dunia kwa asilimia 30 kwa miaka mingi mfululizo.

Amesisitiza kuwa, katika zama hizi za leo, uchumi wa dunia unachanganyika, na maslahi ya nchi mbalimbali zinahusiana, na China itachukulia miaka 20 tangu ijiunge na WTO kama mwanzo mpya, na kuendelea kuhimiza ujenzi wa jumuiya yenye hatma ya pamoja ya binadamu wote.