China yasisitiza kupinga mawasiliano rasmi kati ya Marekani na Taiwan
2021-11-10 15:18:16| Cri

China imepinga vikali mawasiliano rasmi na makubaliano ya aina yoyote ya kijeshi kati ya Marekani na Mkoa waTaiwan.

Msemaji wa Ofisi ya Masuala ya Taiwan ya Baraza la Serikali la China Zhu Fenglian. ametoa kauli hiyo akijibu swali kuhusu habari kuwa wabunge wa Marekani akiwemo seneta John Cornyn waliwasili Taiwan kwa ndege ya kijeshi na kupanga kukutana na mkuu wa mkoa huoTsai Ing-wen.

Amewataka wabunge hao kufuata sera ya kuwepo kwa China moja na taarifa tatu za pamoja kati ya China na Marekani, na kuwaonya kuwa kutoa ishara kwa makosa kwa watu wanaotafuta “uhuru wa Taiwan”, kunaweza kuharibu zaidi amani na utulivu katika Mlango Bahari wa Taiwan.