Kampuni nyingi kushiriki tena kwenye CIIE mwakani
2021-11-11 10:10:43| CRI

Kampuni nyingi kushiriki tena kwenye CIIE mwakani_fororder_VCG111356939870

Maonesho ya nne ya Kimataifa  ya Uagizaji Bidhaa kutoka nje ya China (CIIE) yamefungwa.

Takwimu zinaonesha kuwa mauzo kwenye maonesho hayo yamefikia dola bilioni 70.72 za Kimarekani, na kampuni nyingi zimesema zitashiriki tena kwenye maonesho hayo mwakani.

Habari zilizotolewa na Gazeti la “Russian News” la Russia zimesema, a kampuni moja ya chakula ya Russia imepata faida ya mamilioni ya fedha ilipouza bidhaa zake kwenye maonesho ya CIIE. Gazeti la Lianhezaobao la Singapore limetoa ripoti ikisema, matajiri wengi wa China wametoa fursa maalumu kwa kampuni za Singapore, hivyo zimeshiriki kwenye Maonyesho hayo licha ya changamoto ya COVID-19.

Kati ya makubaliano zaidi ya 200 yaliyofikiwa kwenye maonesho hayo, mengi ni kati ya China na nchi zilizojiunga na pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja”, zikiwemo nchi 33 zilizo nyuma zaidi kimaendeleo duniani.

Kwa upande wa nchi za magharibi, idadi ya kampuni za Marekani zilizoshiriki kwenye Maonyesho ya mwaka huu ilifikia 200, ikiwa ni nyingi zaidi kuliko zamani. Serikali ya Australia haikushiriki kwenye maonesho hayo, lakini kampuni nyingi kutoka jimbo la Victoria la nchi humo zilishiriki.