Rais wa China atoa upongezi kwa rais mpya wa Cape Verde
2021-11-11 09:02:04| cri

 

 

Rais Xi Jinping wa China jana amempongeza rais Jose Maria Neves wa Cape Verde kwa kuchaguliwa kuwa rais mpya wa nchi hiyo.

Rais Xi amesema, China na Cape Verde zina uhuisano wa kirafiki wa muda mrefu, na ushirikiano kati ya nchi hizo mbili umepata mafanikio makubwa yaliyowanufaisha wananchi wao. Baada ya mlipuko wa COVID-19, China na Cape Verde zimesaidiana na kupambana na janga kwa pamoja.

Rais Xi amesema anatilia maanani sana kukuza uhusiano na Cape Verde, na anapenda kushirikiana na rai Neves kusukuma mbele zaidi uhuisiano kati ya nchi hizo mbili.