China na Martekani zatoa taarifa ya pamoja kuhusu kuimarisha hatua za kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa
2021-11-11 08:24:34| CRI

China na Marekani zimetoa Azimio la Glasgow kuhusu Kuimarisha Hatua za Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi, wakati mkutano wa 26 wa Nchi zilizosaini Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (COP26) ukiendelea mjini Glasgow.

Pande hizo mbili zimesema zinapongeza kazi zilizofanyika mpaka sasa, na kuahidi kuendelea kufanya kazi pamoja na pande nyingine ili kuimarisha utekelezaji wa Makubaliano ya Paris.

Pia pande hizo mbili zimekubaliana kuanzisha kikosi kazi kitakachoshughulika na kuboresha hatua za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi ili kuboresha ushirikiano katika suala hilo kati ya nchi hizo mbili na mchakato wa pande nyingi.