China na Marekani zafikia Azimio la pamoja la kuimarisha operesheni za tabianchi
2021-11-11 11:50:43| Cri

China na Marekani tarehe 10 mwezi Novemba zimetangaza “Azimio la pamoja la Glasgow linalohusu kuimarisha operesheni za tabianchi kati ya China na Marekani katika miaka ya 2020 ya karne ya 21” kwenye kikao cha Mkutano wa mabadiliko ya tabianchi wa Umoja wa Mataifa unaofanyika mjini Glasgow huko Scotland.

China na Marekani zimesifu kazi zao zinazozifanya, na kuahidi kuwa zitaendelea kufanya juhudi na kuimarisha utekelezaji wa “Makubaliano ya Paris”. Zaidi ya hayo, chini ya msingi wa hali halisi zitaimarisha operesheni za tabianchi na kukabiliana na mgogoro wa tabianchi. Pande zote mbili zimekubali kuunda “Timu ya kazi ya kuimarisha operesheni za tabianchi katika miaka ya 2020 ya karne ya 21”, na kuhimiza ushirikiano na mchakato wa pande nyingi juu ya mabadiliko ya tabianchi kati ya nchi hizo mbili.