Rais wa China ahutubia mkutano wa APEC
2021-11-11 09:37:20| CRI

Rais wa China ahutubia mkutano wa kilele wa Wakurugenzi wa Viwanda na Biashara wa APEC_fororder_32fa828ba61ea8d3b8ee675777cd5747271f58e1

Rais Xi Jinping wa China amehutubia mkutano wa kilele wa viongozi wa viwanda na biashara wa Shirika la Ushirikiano wa Uchumi la Asia na Pasifiki kwa njia ya mtandao.

Katika hotuba yake, rais Xi amesema, janga la COVID-19 bado linaenea duniani, na nchi za Asia na Pasifiki zinapaswa kubeba majukumu ya kizama, kufanya kazi ya uongozi, na kusonga mbele kithabiti kwa lengo la kujenga jumuiya yenye hatma ya pamoja ya kanda ya Asia na Pasifiki.

Pia rais Xi ametoa mapendekezo manne, ambayo ni kupambana na janga la COVID-19 kwa nguvu zote, kushikilia kufungua mlango na ushirikiano, kubadilisha njia ya maendeleo ili kupunguza uchafuzi wa mazingira, na kuhamasisha uvumbuzi.