Kikao cha 6 cha wajumbe wote cha Kamati Kuu ya 19 ya CPC chafungwa
2021-11-11 20:20:19| Cri

Kikao cha 6 cha wajumbe wote cha Kamati Kuu ya 19 ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) kimefanyika kuanzia Novemba 8 hadi 11 mjini Beijing, ambapo kilipitisha taarifa tarehe 11.

Kikao hiki kilisikiliza na kujadili ripoti ya kazi iliyotolewa na rais Xi Jinping kwa niaba ya Ofisi ya Kisiasa ya Kamati Kuu ya CPC, kujadili na kupisha Azimio la Kamati Kuu hiyo kuhusu Mafanikio Makubwa na Uzoefu wa Kihistoria Zilizopatikana katika Miaka Mia Moja Iliyopita, pamoja na Azimio kuhusu kuitisha Mkutano wa 20 wa wajumbe wote wa Chama hicho. Rais Xi alifanya ufafanuzi kuhusu rasimu ya Azimio la Kamati Kuu ya CPC kuhusu Mafanikio Makubwa na Uzoefu wa Kihistoria Zilizopatikana katika Miaka Mia Moja Iliyopita.

Kikao hiki kimeeleza kuwa, katika miaka mia moja iliyopita, Chama hicho kimewaongoza wananchi kufanya juhudi kubwa, na kukusanya uzoefu wenye thamani kubwa wa kihistoria, ikiwa ni pamoja na kushikilia uongozi wa Chama cha Kikomunisti cha China, kutanguliza maslahi ya wananchi, kufanya uvumbuzi wa kinadharia, kudumisha uhuru na kujiamulia mambo, kushikilia njia yenye umaalumu wa China, kutupilia macho dunia, kufanya uvumbuzi, kuthubutu kufanya mapambano, kushikilia mstari wa pamoja wa mapambano, na kujifanyia mapinduzi. Huo ni uzoefu uliopatikana katika mazoezi ya muda mrefu ambao unatakiwa kuthaminiwa, ni utajiri wa kiroho zilizofanywa kwa pamoja na Chama na watu, ni lazima zithaminiwe na kudumishwa kwa muda mrefu, na kuzidi kukuzwa katika mazoezi ya zama mpya.