Mke wa rais wa China ahojiwa na jarida la Courier la UNESCO
2021-11-11 08:22:24| CRI

Mke wa rais wa China, ambaye pia ni mjumbe maalumu wa UNESCO kuhusu elimu wa watoto wa kike na wanawake Bibi Peng Liyuan amehojiwa na jarida la Courier la UNESCO.

Bibi Peng amesema, kutokomeza umaskini na kutimiza usawa wa kijinsia ni lengo la pamoja la binadamu, pia ni matumaini ya pamoja ya wanawake kote duniani. Amesema China imetimiza lengo la kutokomeza umaskini uliokithiri, huku elimu ikiwa ni hatua muhimu sana ya kupunguza umaskini.

Amesema kuwa, inapaswa kuimarisha nia ya kuhimiza elimu kwa watoto wa kike na wanawake na kujitahidi kuwasaidia wanawake wengi zaidi wapate elimu bora, illi kutoa mchango kwa ajili ya kutimiza lengo la mwaka 2030 la Maendeleo Endelevu la Umoja wa Mataifa.

Mwaka huu ni maadhimisho ya miaka 75 tangu UNESCO kuanzishwa, jarida la Courier limetoa toleo maalumu ya kufuatilia changamoto inayoikabli elimu ya dunia kwa sasa na utatuzi wake.