Balozi wa China UN asema kauli peke yake haziwezi kusaidia kutatua changamoto ya mabadiliko ya tabia nchi
2021-11-11 15:25:31| Cri

Mjumbe wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa (UN), Balozi Zhang Jun, amesema kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi kunahitaji kujitolea kwa umadhubuti na kuendelea kuchukua hatua, na si kutoa kauli mbiu tupu na maneno matupu.

 

Kwenye ujumbe aliotoa kwa njia ya Twitter, Balozi Zhang ameongeza kuwa dunia haihitaji sera zinazobadilika mara kwa mara, magari ya kifahari na wapambe, au kuhatarisha afya za watu wengi bila kuwajibika. Balozi Zhang amesema hayo wakati ripoti za vyombo vya habari zinasema Rais Joe Biden wa Marekani alitumia msafara wa magari 85 kupita Roma kabla ya mkutano wa kilele wa hali ya hewa wa COP26.

 

Balozi Zhang amesema China imekuwa ikiunga mkono kwa dhati hatua za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi, na haikujitoa kwenye makubaliano ya Paris. Amesema Marekani imerudi nyuma mara kwa mara kwenye sera zake kuhusu mabadiliko ya tabia nchi, na kuitaka iache kuzilaumu nchi nyingine, iwajibike na ichukue hatua madhubuti.