Ushirikiano kati ya China na Marekani ni chaguo pekee sahihi
2021-11-12 09:19:53| CRI

Mjumbe maalumu wa mabadiliko ya tabianchi wa China Bw. Xie Zhenhua amesema, kutolewa kwa azimio la pamoja kati ya China na Marekani kuhusu kuimarisha hatua za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi katika karne 21 kunaonyesha kwa mara nyingine tena kwamba, ushirikiano kati ya nchi hizo ni chaguo pekee sahihi, na unaweza kufanikisha mambo yanayonufaisha nchi hizo mbili na dunia nzima.

Akizungumza na waandishi wa habari, Xie Zhenhua amesema mabadiliko ya tabianchi ni changamoto ya pamoja ya binadamu wote, na yanahusiana na maslahi ya vizazi vya baadaye. Amesema China na Marekani zina maoni ya pamoja kuhusu suala hilo kuliko mgongano, na zina uwezo mkubwa wa kushirikiana, na anatumai azimio hilo linaweza kutoa mchango kwa ajili ya mkutano wa 26 wa Pande zilizosaini Mkataba wa Bioanuwai.

Kwa upande wa Marekani, mwakilishi maalumu wa rais wa Marekani John Kerry amesema, ingawa Marekani na China zina maoni ya tofauti, lakini ushirikiano ni njia pekee ya kufanikisha suala la mabadiliko ya hali ya hewa.