Watu 40 hawajulikani walipo baada ya ajali ya boti mashariki mwa DRC
2021-11-12 08:46:04| cri

Watu zaidi ya 40 hawajulikani walipo baada ya ajali ya boti iliyotokea jana asubuhi katika eneo la Kalehe, jimbo la Kivu Kusini, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Tathmini ya awali iliyotolewa na mkuu wa shirika la kiraia katika eneo hilo Bw. Delphin Birimbi, watu 57 wamenusurika na miili minane tayari imepatikana.

Habari zinasema, mpaka sasa, chanzo cha ajali hiyo bado hakijajulikana na kazi za uokoaji inaendelea