Marais wa China na Rwanda watumiana salamu za pongezi kuadhimisha miaka 50 ya uhusiano wa kibalozi kati ya nchi zao
2021-11-12 10:59:32| Cri

Rais Xi Jinping wa China na mwenzake wa Rwanda Paul Kagame jana Alhamis walitumiana salamu za pongezi ili kuadhimisha miaka 50 ya uhusiano wa kibalozi kati ya nchi zao.

Rais Xi amesisitiza kuwa anatilia maanani kukuza uhusiano kati ya China na Rwanda, na anapenda kushirikiana na rais Kagame na kutumia vizuri fursa ya maadhimisho ya miaka 50 ya uhusiano wa kibalozi na mkutano ujao wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC, katika kuinua kiwango cha kuaminiana kisiasa, na kuimarisha ushirikiano wa sekta zote kwenye ujenzi wa pamoja wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja”, ili kusukuma mbele maendeleo ya uhusiano wa nchi hizo mbili na kuwanufaisha wananchi wao.

Kwa upande wake, rais Kagame amesema, China imeiunga mkono Rwanda kupitia majukwaa mbalimbali ikiwemo FOCAC na “Ukanda MMoja, Njia Moja”, na kutoa mchango mkubwa katika mageuzi ya Rwanda. Rwanda inapenda kuendelea kupanua wigo wa ushirikiano kati yake na China.