Mkutano wa 6 wa wajumbe wote wa Kamati Kuu ya 19 ya CPC wafungwa
2021-11-12 08:57:26| CRI

Mkutano wa 6 wa wajumbe wote wa Kamati Kuu ya 19 ya CPC wafungwa_fororder_1128055386_16366350314791n

Mkutano wa 6 wa wajumbe wote wa Kamati Kuu ya 19 ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) umefungwa jana mjini Beijing.

Mkutano huo umesisitiza kuwa tangu mkutano wa 18 wa Kamati Kuu ya Chama, Ujamaa wenye Umaalum wa China umeingia katika zama mpya, na Kamati Kuu ya CPC inayoongozwa na rais Xi Jinping imehimiza Chama na taifa kupata mafanikio na mageuzi makubwa ya kihistoria.

Mkutano huo umesema katika zama mpya, mfumo wa uongozi wa CPC umekamilika siku hadi siku, nguvu ya taifa ya China imeongezeka zaidi, maisha ya wananchi yameboreshwa, na uhifadhi wa mazingira umepiga hatua kubwa.

Mkutano huo umesema Chama kimethibitisha hadhi ya rais Xi ya kuwa kiini cha kamati kuu ya chama na chama kizima, pia kuthibitisha hadhi ya uongozi wa wazo la rais Xi Jinping la Ujamaa wenye Umaalumu wa China katika zama mpya, ambalo lina una umuhimu mkubwa kwa maendeleo ya Chama na shughuli za taifa, na mchakato wa ustawishaji mkubwa wa taifa la China.